• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping azitaka nchi mbalimbali zifanye juhudi za kuhimiza ushirikiano wa kufungua mlango na kutimiza maendeleo kwa pamoja

    (GMT+08:00) 2018-11-05 10:41:04

    Rais Xi Jinping leo huko Shanghai ametoa wito wa kuzitaka nchi mbalimbali zioneshe ujasiri zaidi na kufanya juhudi za kuhimiza ushirikiano wa kufungua mlango, na kutimiza maendeleo kwa pamoja.

    Rais Xi amesema, hivi sasa uchumi wa dunia unafanyiwa marekebisho kwa kina, uendelezaji wa uchumi wa upande mmoja umeibuka sasa, utandawazi wa uchumi duniani unakumbwa na matatizo, ushirikiano wa pande mbalimbali na utaratibu wa biashara huria vimekumbwa na pigo, ambapo hali isiyotulia na isiyotazamiwa bado ziko nyingi, watu wanatakiwa kufuata kanuni, kutambua hali ya jumla ya mambo, kuongeza nia thabiti ya kufanya ushirikiano wa kufungua mlango, ili kukabiliana pamoja na hatari na changamoto.

    Rais Xi amesisitiza, utandawazi wa uchumi duniani ni wimbi kuu la historia ambalo halibadiliki, kufanya ushirikiano wa kufungua mlango ni nguvu kubwa ya kuimarisha uhai wa uchumi na biashara wa kimataifa, ni matakwa halisi ya sasa katika kuhimiza utulivu na ufufukaji wa uchumi wa dunia, na ni matakwa ya zama hizi ya kuhimiza jamii ya binadamu iendelee siku hadi siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako