• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atoa mapendekezo ya kuhimiza ufunguaji mlango na ushirikiano

  (GMT+08:00) 2018-11-05 11:44:17

  Rais Xi Jinping wa China leo huko Shanghai amezihimiza nchi mbalimbali duniani kufungua mlango, kuongeza ushirikiano wa kunufaishana, kuweka kipaumbele katika uvumbuzi, kuharakisha mabadiliko ya injini za uchumi, kushikilia shirikishi na kunufaisha pande mbalimbali, na kuhimiza maendeleo ya pamoja.

  Rais Xi amesema nchi zote zinapaswa kuwa na msimamo wazi wa kupinga vitendo vya kujilinda kibiashara na vya upande mmoja, kuinua kiwango cha kufungua mlango kati ya pande mbilimbili na pande nyingi, kuhimiza mawasiliano na mafungamano ya uchumi, kujenga kwa pamoja uchumi wa kufungua mlango duniani, kuongeza uratibu wa sera za uchumi ili kupunguza athari ya changamoto ya ndani kwa nje, kuhimiza ujenzi wa utaratibu ulio wa usawa, haki na uwazi wa biashara ya kimataifa, kuongeza shughuli za biashara na uwekezaji huria na kuzirahisisha, na kuhimiza uchumi wa dunia kufunguliwa, kuwasiliana, na kufungamana zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako