• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa sera za kuhimiza Shanghai na sehemu nyingine kufungua mlango zaidi

  (GMT+08:00) 2018-11-05 11:44:40

  China leo imetangaza kutoa sera tatu ili kuhimiza Mji wa Shanghai na sehemu nyingine kufungua mlango zaidi.

  Rais Xi Jinping wa China leo huko Shanghai amesema, China itaongeza eneo jipya kwenye maeneo ya majaribio ya biashara huria mjini Shanghai, ili kuhamasisha na kuunga mkono mji huo kukusanya uzoefu wa kuhimiza shughuli za uwekezaji na biashara huria na kuzirahirisha, na kueneza uzoefu huo kwa sehemu nyingine nchini China. Pia China itajaribu kutekeleza utaratibu wa kuandikisha makampuni ya teknolojia katika soko la hisa la Shanghai. Aidha, China itaunga mkono utandawazi wa maendeleo ya mji wa Shanghai na mikoa ya Zhejiang na Jiangsu, na kuuweka kwenye mpango wa kimkakati wa taifa la China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako