• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China inatia nguvu mpya katika kuendeleza pamoja uchumi wa dunia ulio wa kufungua mlango

  (GMT+08:00) 2018-11-05 16:41:23

  Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje yamefunguliwa leo huko Shanghai, ambapo nchi, sehemu na mashirika ya kimataifa 172 pamoja na kampuni zaidi ya 3,600 zimeshiriki kwenye maonesho hayo.

  Kwenye ufunguzi wa maonesho hayo, Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba ya "Kujenga pamoja uchumi wa dunia wa kufungua mlango ulio wa kufanya uvumbuzi na ushirikiano wa pande nyingi", pia ametoa mapendekezo matatu ya kuhimiza nchi mbalimbali kufungua mlango na kufanya ushirikiano, na kutangaza hatua tano za China za kuongeza nguvu ya kufungua mlango zaidi. Mapendekezo na hatua hizo zimetia nguvu kubwa zaidi kwa utetezi wa daima wa China kuhusu kulinda pamoja mfumo wa biashara huria na biashara ya pande mbalimbali, kujenga pamoja uchumi wa dunia wa kufungua mlango, na kuijenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

  Katika hotuba yake, Rais Xi ameeleza kuwa utandawazi wa uchumi duniani ni wimbi kuu la kihistoria ambalo halibadiliki, na kufungua mlango na kufanya ushirikiano ni nguvu kubwa ya kuimarisha uhai wa uchumi na biashara ya kimataifa, ufafanuzi wake unasaidia watu watambue mwelekeo wa kujiendeleza katika hali ya sasa yenye utata. Rais Xi amezitaka nchi mbalimbali zioneshe ujasiri zaidi katika kushikilia kufungua mlango na kufungamana, kupanua nafasi ya ushirikiano wa kunufaishana, na kushikilia kuufanya uvumbuzi uongoze maendeleo. Pia kuharakisha kubadilishana kwa uwezo mpya na uwezo wa zamani, kushikilia ushirikiano na kuleta manufaa kwa pande nyingi, na kusukuma mbele maendele ya pamoja ya nchi mbalimbali. Mapendekezo hayo yameonesha nia ya dhati ya China ya kupenda kushirikiana na nchi mbalimbali katika kutimiza maendeleo kwa pamoja.

  Watu wanaona kuwa, "kufungua mlango, kufanya uvumbuzi, na kufanya ushirikiano wa pande nyingi" ni maneno muhimu yaliyotiliwa maanani sana kwenye hotuba ya rais Xi. Hayo ni majumuisho ya hali ya juu kuhusu uzoefu wa China wa miaka 40 katika mageuzi na kufungua mlango, pia ni masharti yasiyokosekana kwa China katika kutimiza maendeleo ya sifa ya juu katika siku za baadaye.

  Jambo linalofutiliwa zaidi na watu ni kwamba, katika hotuba yake, Rais Xi ameahidi kuadhibu kithabiti vitendo vya kukiuka haki na maslahi ya wafanyabiashara wa nje walioko nchini China, hasa ni vitendo vya kukiuka hakimiliki ya ubunifu, kuinua sifa na ufanisi wa kuthibitisha hakimiliki ya ubunifu, na kuingiza utaratibu wa adhabu ya kutoa fidia, ili kuongeza gharama za kuvunja sheri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako