• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atangaza hatua mpya za China katika kufungua mlango kwenye ufunguzi wa CIIE

    (GMT+08:00) 2018-11-05 16:49:26

    Rais Xi Jinping wa China amehudhuria na kutoa hotuba kwenye Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China yaliyofunguliwa leo mjini Shanghai. Rais Xi ametangaza kuwa China itaongeza hatua za kufungua mlango, akisisitiza kuwa mafungamano ya kiuchumi duniani ni mwelekeo usiozuilika, nchi zote zinatakiwa kuhimiza ufunguaji mlango na ushirikiano, ili kupata maendeleo kwa pamoja. Pia amesisitiza kuwa China haitasimamisha hatua zake katika kuhimiza ufunguaji mlango katika kiwango cha juu zaidi, kujenga uchumi ulio wazi kwa dunia, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Maonesho ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China ni maonesho ya kwanza ya kitaifa yanayohusu uagizaji wa bidhaa duniani, ambayo yanafanyika kwa kufuata pendekezo la rais Xi Jinping wa China. Maonesho hayo ya kwanza yameshirikisha nchi, sehemu na mashirika ya kimataifa 172, viwanda zaidi ya 3,600 duniani, pamoja na wafanyabiashara zaidi ya laki 4 kutoka China na nchi za nje.

    Rais Xi Jinping akihutubia ufunguzi wa maonesho hayo, ameeleza kuwa kufanyika kwa maonesho hayo ni uamuzi muhimu wa China katika kuhimiza ufunguaji mlango kwa kiwango cha juu zaidi, pia ni hatua muhimu ya China ya kufungua soko kwa dunia nzima. Rais Xi anasema:

    "Kufanyika kwa maonesho haya kumeonesha msimamo wa China wa kuunga mkono utaratibu wa biashara ya pande nyingi, na kuhimiza biashara huria, pia ni hatua halisi ya China katika kuhimiza ujenzi wa uchumi wa kufungua mlango kwa dunia, na kuunga mkono mafungamano ya kiuchumi duniani. Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya 'Karne mpya, na kunufaika kwa pamoja katika siku za baadaye', yanawakaribisha marafiki wa nchi mbalimbali kutumia fursa hii nzuri, kukuza ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi na kibiashara, ili kutimiza ustawi na maendeleo kwa pamoja."

    Hivi sasa utaratibu wa pande nyingi na biashara huria unakabiliwa na changamoto mbalimbali. Rais Xi ametoa mapendekezo kwa pande mbalimbali kutambua hali halisi ya dunia, na kushikilia imani ya kufungua mlango na kufanya ushirikiano. Akisema:

    "Nchi mbalimbali zinatakiwa kushikilia kufungua mlango na kufanya mawasiliano, na kupanua maeneo ya ushirikiano wa kunufaishana, wakati huo huo zinapaswa kupinga kithabiti kujilinda kibiashara, utaratibu wa upande mmoja, na kujenga kwa pamoja uchumi wa dunia wa kufungua mlango, kusukuma mbele biashara huria na uwekezaji. Pia zinatakiwa kutoa kipaumbele katika uvumbuzi, na kubadilisha msukumo wa zamani wa kiuchumi. Vilevile zinatakiwa kuhimiza mafungamano ya kiuchumi duniani kupata maendeleo kwa kufungua mlango zaidi, kuwa na uvumilivu, kuwanufaisha watu wengi zaidi, ili kuwafanya watu wa nchi mbalimbali kunufaika kwa pamoja katika mchakato wa mafungamano ya kiuchumi, na ongezeko la uchumi duniani."

    Huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango. Rais Xi amesisitiza kuwa China itatekeleza kwa hatua madhubuti mkakati wa kufungua mlango wa kunufaishana, na kwamba China siku zote ni msukumo muhimu katika kufungua mlango kwa dunia nzima na kuhimiza ongezeko la uchumi duniani, pia mchangiaji muhimu katika mageuzi ya usimamizi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako