• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SERIKALI YA KITAIFA YA UGANDA YAKUSANYA MABILIONI YA USHURU KUTOKA KWA HUDUMA YA PESA KWA NJIA YA SIMU

    (GMT+08:00) 2018-11-05 19:40:35
    Halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Uganda (URA), imekusanya shilingi bilioni 103, pesa za Uganda kutoka kwa huduma ya pesa kwa njia ya simu.

    URA imekusanya pesa hizo katika kipindi cha robo ya mwaka wa kifedha wa 2018/2019, hii ikiwa ni kati ya mwezi Julai na mwezi Septemba.

    Hata hivyo, pesa hizi ni chini ya matarajio ya serikali, ambako bilioni 151.5 pesa za Uganda zilikuwa zikusanywe kwa kipindi hiki.

    Kutoza ushuru huduma ya pesa kwa njia ya simu ulianzishwa mwezi Julai mwaka huu, kama njia moja ya kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi.

    Halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Uganda-URA inatarajia kukusanya takriban shilingi trilioni 16, pesa za Uganda, kwenye kipindi cha fedha cha mwaka wa 2018/2019.

    Hata hivyo, kulingana na mkurugenzi mkuu wa mawasiliano wa URA Bwana Ian Rumanyika, huenda ushuru uliokusanywa kutoka kwa huduma ya pesa kwa njia ya simu ulikuwa wa chini kwa sababu ya kupunguzwa kwa asilimia ya ada inayotozwa kutoka asilimia moja hadi asilimia 0.5. Mageuzi haya yalifanywa mwezi Septemba mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako