• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikosi cha awali kitakachoshiriki mashindano ya Cecafa vijana chatangazwa Z'bar

  (GMT+08:00) 2018-11-06 09:51:21
  Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Salum Ali Haji, ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 38, kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Cecafa ya vijana yanayotarajiwa kufanyika nchini Uganda Disemba 15-25 mwaka huu .

  Kocha Salum ametangaza kikosi hicho kwenye ukumbi wa uwanja wa Amaan, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana mchana.

  Wachezaji hao watafanyiwa mchujo na kubakisha wachezaji 25 kuunda timu ya Taifa ya U20 ya Zanzibar.

  Aidha kocha Salum Ali amesema wachezaji hao waje na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa wawe wamezaliwa January mwaka 2000 ili kupata umri sahihi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako