• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Peng Liyuan akutana na Bill Gates

  (GMT+08:00) 2018-11-06 10:17:25

  Mke wa rais wa China Bibi Peng Liyuan, ambaye ni balozi wa heshima wa Shirika la Afya Duniani kuhusu maradhi ya kifua kikuu na UKIMWI na Bw. Bill Gates, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa Mfuko wa Bill&Melinda Gates wamekutana mjini Shanghai.

  Bibi Peng amesema kwa muda mrefu Mfuko wa Bill&Melinda Gates umefanya ushirikiano mzuri na idara husika za China katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI, kupunguza umaskini katika sekta ya huduma za afya, na ujenzi wa uwezo katika afya ya umma duniani.

  Bw. Gates amepongeza hotuba muhimu iliyotolewa na rais Xi Jinping katika ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Bidhaa Zinazoingizwa na China, na kusema China inastahili pongezi kutokana na kufuata kanuni za uwazi, ujumuishi, pamoja na manufaa na mafanikio kwa pande zote. Bilionea huyu wa Marekani aliyejikita katika mambo ya hisani ameongeza kuwa mfuko wake unapenda kuendelea kushirikiana na China katika mambo ya hisani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako