• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje yameonesha nia thabiti ya China kuzifungulia mlango nchi za nje

    (GMT+08:00) 2018-11-06 16:19:57

    Kwenye Mkutano wa Baraza la vyombo vya habari vya mambo ya fedha na uchumi na Jumuiya ya washauri bingwa uliofanyika alasiri ya tarehe 5, Mkuu wa Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha taifa Bw. Shen Haixiong alipotoa hotuba alisema, Rais Xi Jinping alitoa hotuba kwenye ufunguzi wa Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje, maneno yanayoleta matumaini kwenye hotuba yake, yamefuatiliwa mara moja kwenye mtandao, na kukubaliwa sana na watu wa ndani na nje ya nchi.

    Bw. Shen Haixiong amesema, hotuba aliyotoa Rais Xi imefafanua sera na hatua za China za kufungua mlango, na kueleza nia ya dhati ya China ya kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja na nchi mbalimbali duniani, maelezo yake yameonesha vilivyo China ni nchi inayowajibika. Na maneno aliyotaja kwenye hotuba yake, kama vile "Bahari kubwa, "Kwaya", na "Tochi", mara moja yamefuatiliwa sana kwenye mtandao wa internet, na kuzungumzwa sana na watu wa ndani na nje ya nchi. Maonesho hayo makubwa ya kwanza duniani kuhusu bidhaa zinazoingizwa kutoka nchi mbalimbali, yameonesha hiari na hamasa ya China kufungua soko kwa dunia, na kueleza matumaini ya dhati ya China ya kuzikaribisha nchi mbalimbali zishiriki na kunufaika na fursa mpya wa maendeleo ya China.

    Bw. Shen Haixiong amesema, wiki moja iliyopita, Rais Xi Jinping alitoa hotuba mkoani Guangdong akieleza tena nia thabiti na imani kubwa kwa dunia nzima, kwamba mageuzi ya China hayatasita, na hatua za kufungua mlango hazitasita, na China inapenda kunufaika pamoja na dunia kwa fursa ya maendeleo ya China. Na hotuba aliyotoa Rais Xi kwenye maonesho makubwa yanayofanyika Shanghai imeonesha kuwa China itapanua kwa kina kazi yake ya kufungua mlango.

    Kwenye mkutano huo, Bw. Shen Haixiong amevitaka vyombo vya habari vya nchi mbalimbali vifuatilie mapendekezo ya nchi zenye soko jipya na nchi zinazoendelea, na visikilize kwa uvumilivu sauti za nchi dhaifu, ili vitoe habari na kusaidia maingiliano na mafungamano kati ya nchi zenye utamaduni na staarabu tofauti.

    Bw. Shen Haixiong amesema, kutoa habari ni lazima kufuatilie hali ya mambo ya hivi sasa. Vyombo vya habari vya dunia na watu wengi wanafuatilia sana Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje na kufuatilia mapendekezo ya China, hali hii imeonesha kihalisi, kwamba kuunga mkono kufanya ushirikiano wa pande nyingi na biashara huria, bado ni sauti kuu ya jumuia ya kimataifa. Wimbi la zama hizi halizuiliki, tukiwa wanahabari, tunatakiwa kubeba jukumu letu katika kusukuma kithabiti utandawazi wa uchumi duniani, na kulinda utaratibu wa uchumi wa kimataifa ulio wa usawa na kufungua mlango.

    Kuhusu masuala ya kupinga utandawazi wa uchumi duniani na kutokea kwa mawazo yanayokwenda kinyume, utandawazi wa uchumi duniani unakabiliwa na changamoto kubwa sana, Bw. Shen Haixiong anaona vyombo vya habari vinatakiwa kutetea ushirikiano wa pande nyingi na shirikishi, kuepusha hali ya kukabiliana na kupambana, kujenga mazingira ya mawazo ya kutafuta maoni ya pamoja na kuweka kando maoni tofauti, kutafuta maoni ya pamoja na kuheshimu maoni tofauti, na kutafuta maoni ya pamoja ili kuondoa maoni tofauti, ili kuleta hali ya matumaini kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa dunia nzima. Amesisitiza kuwa, vyombo vya habari vya nchi mbalimbali ni lazima viwe walinzi wa mfumo wa uchumi wa kufungua mlango na kuzitia moyo pande mbalimbali zenye maslahi tofauti ziimarishe mazungumzo na mashauriano. Utaratibu wa uchumi wa kimataifa ulio wa usawa na halali ni vigumu kusukumwa mbele, ila tu nchi zote zifuate mtazamo wa kufanya mashauriano, kujenga na kunufaika pamoja ili kuendeleza uchumi wa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako