• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na dunia zatakiwa kujenga kwa pamoja daraja la kutafuta ustawi

    (GMT+08:00) 2018-11-07 16:53:10

    Wiki hii rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China, akitoa wito wa kujenga kwa pamoja uchumi shirikishi unaofanya uvumbuzi na kufungua mlango, na kusisitiza kuwa China itachukua hatua tano muhimu za kupanua ufunguaji mlango, kuhimiza uwezo wa kuagiza bidhaa kutoka nje, na kuzidi kulegeza masharti ya kuingia kwenye soko. Baada ya hapo waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza tena China itahimiza maendeleo yenye kiwango cha juu zaidi na sifa bora zaidi.

    Msukumo wa China wa kufungua mlango na kufanya ushirikiano wa kimataifa unatokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango, uliokuwa ukiendelea katika miaka 40 iliyopita. Katika kipindi hicho, wastani wa mapato ya wachina umeongezeka mara 25, pato la taifa GDP limeongezeka mara mbili kila baada ya miaka minane, na watu zaidi ya milioni 700 wameondokana na umaskini, kiasi ambacho kinachukua asilimia 70 ya idadi ya watu maskini duniani, na kuchangia sana maendeleo ya dunia.

    Ufunguaji mlango wa China si kama tu unahimiza maendeleo yake yenyewe, bali pia umeinufaisha dunia nzima. Siku hizi shughuli mbalimbali za ushauri, biashara na kusainiwa kwa makubaliano kunaendelea katika Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China CIIE, na mwelekeo wa uchumi wa China umebadilika kutoka kutegemea zaidi uuzaji bidhaa nje kuwa kutegemea zaidi matumizi ya fedha katika soko la ndani. Serikali ya China inakadiria kuwa, katika miaka 15 ijayo, thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya China na utoaji wa huduma itazidi dola trilioni 30 za kimarekani, na dola trilioni 10 za kimarekani mtawalia.

    Mkurugenzi wa Shirika la fedha la Kimataifa IMF Bibi Christine Lagarde anaona China inajenga daraja linaloelekea kwenye ustawi. Katika robo tatu za mwanzo mwaka huu, matumizi ya fedha yalichangia asilimia 78 ya ongezeko la GDP la China, na kiasi hicho kilikuwa asilimia 50 tu katika miaka mitano iliyopita. Ujenzi wa daraja hilo si kama tu ni mahitaji ya wachina, bali pia ni mahitaji ya dunia. Ingawa uchumi wa China unakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile hali isiyotabirika ya uchumi wa dunia, na kufufua kwa hali ya kujilinda kibiashara, lakini mwelekeo wa jumla wa kupata ongezeko haubadiliki.

    China inaahidi kuwa, siku zote itakuwa muungaji mkono wa kufungua mlango kwa pamoja duniani, msukumo muhimu wa ongezeko la dunia, soko kubwa kwa nchi mbalimbali kupanua fursa za biashara, pamoja na mchangiaji muhimu wa mageuzi na usimamizi wa dunia. Ili kujenga kwa pamoja dunia nzuri zaidi, nchi zote zinatakiwa kuonesha ushupavu mkubwa zaidi, na kuhimiza kwa nguvu ufunguaji mlango na ushirikiano, ili kutimiza maendeleo ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako