• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Zambia nchini China asema CIIE ni fursa ya maendeleo kwa kampuni ndogo na za ukubwa wa kati nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-11-07 18:42:34

    Balozi wa Zambia nchini China Bi. Winnie Natala Chibesakunda leo huko Shanghai amesema, maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China CIIE yametoa fursa ya maendeleo kwa kampuni ndogo na za ukubwa wa kati nchini humo, vilevile yatahimiza mchakato wa utandawazi wa viwanda wa nchi hiyo. Anasema,

    "Kampuni nyingi za Zambia zimeshiriki kwenye maonesho ya uagizaji bidha ya kimataifa ya China na kuleta bidhaa zao, na kila kampuni inafurahia kupata orodha nyingi za uagizaji bidhaa. Nina imani kuwa kampuni hizo zitaongeza uwezo wa utengenezaji na kiwango cha utandawazi wa viwanda baada ya kurudi Zambia. Kufungua mlango kwa China hakika kutahimiza biashara ya Zambia kwa nje na kuinua kiwango cha utandawazi wa viwanda. "

    Kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka huu hapa Beijing, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuziunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye maonesho hayo, pia kufuta ada ya ushiriki ya nchi zenye matatizo kiuchumi. Bi. Chibesakunda ameishukuru serikali ya China kwa msaada wake. Anasema,

    "Rais Xi Jinping ametimiza ahadi zake. Serikali ya China imetoa msaada kwa pande zote kwa kampuni zetu zinazoshiriki kwenye maonesho hayo. Serikali ya Zambia inafurahi sana na kuishukuru sana serikali ya China. Tutapoteza fursa nzuri ya maendeleo kama tusingepata uungaji mkono wa China."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako