• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sh27b zatengwa kukabiliana na upatikanaji wa soko

  (GMT+08:00) 2018-11-07 18:49:17
  Sera mpya imezinduliwa nchini Uganda ili kukabiliana na changamoto za viwango,uzalishaji mdogo na upatikanaji wa soko miongoni mwa kampuni ndogo na zile za wastani.

  Wakati akizindua mpango huop wa mkakati jijini Kampala,Waziri wa Biashara,Bi Amelia Kyambadde,alisema mojawapo ya sekta kuu ya uchumi haizalishi kama inavyotakikana.

  Hii,alisema,imeitia wasiwasi serikali na kuifanya kutafuta njia ambazo suala hilo linawqeza kushughulikiwa.

  Kyambadde apia alitaja upatikanaji mdogo wa fedha ,gharama za juu za umeme,uwezo mdogo wa uzalishaji,upatikanaji finyu wa soko na changamoto za viwango kama mambo ambayo kampuni ndogo na zile za wastani inazokabiliana nazo.

  Kwa mujibu wa Wizara ya Biashara nchini Uganda,biashara ndogo na za wastani zinawakilisha asilimia 95 ya biashara zote nchini humo.

  Kulingana na Shirika la Takwimu,takriban asilimia 57 ya kampuni ndogo na kati zinaendesha shughuli katika sekta ya biashara,na kuajiri watu zaidi ya milioni 3.5,ambayo ni sawa na asilimia 42 ya ajira zote nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako