Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa, China itashikilia mwongozo wa itikadi ya ujamaa wenye umaalumu wa kichina katika zama mpya na kushikilia utekelezaji wa maamuzi ya kamati kuu ya chama.
Akizungumza kwenye ziara ya ukaguzi mjini Shanghai, rais Xi pia amesisitiza kuimarisha imani na nia katika kufanya mageuzi na ufunguaji mlango, kuharakisha hatua ya kujenga utaratibu wa uchumi wa kisasa, na kuinua uwezo wa kufanya ushindani ili kuchangia katika maendeleo ya mageuzi kote nchini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |