• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi ya mabingwa Ulaya-Matokeo ya mechi za makundi E hadi H

    (GMT+08:00) 2018-11-08 08:46:48

    Baada ya matokeo ya kundi A hadi D mechi zilizochezwa juzi, jana mechi za makundi mengine ziliendelea, ambapo

    kundi E: FB Bayern Munchen imetoka na ushindi wa 2-0 dhidi ya AEK Athens, Benfica wao wametoka sare ya 1-1 na Ajax.

    Nayo Lyon imemaliza kwa sare ya 2-2 na Hoffenheim, huku Manchester city imefanya mauaji kwa kuichapa Shakhtar Donetsk 6-0 katika kundi F.

    kundi G: CSKA Moscow imekubali kipigo cha 2-1 toka kwa Roma, nayo Real Madrid imetoa kipigo cha mbwa mwizi cha 5-0 kwa Victoria Plzen, na michezo ya kundi H, Valencia imeifunga Young Boys 3-1 huku Manchester United ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Juventus.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako