• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vyama vya Democrat na Republican vyadhibiti mabaraza tofauti ya bunge la Marekani

  (GMT+08:00) 2018-11-08 09:44:21

  Chama cha Democrat kimepata udhibiti wa baraza la chini la Bunge la Marekani, huku chama cha Republican kimeendelea kudhibiti baraza la Senate, baada ya matokeo ya upigaji kura uliofanyika jumanne kutangazwa.

  Chama cha Democrat kimepata viti 218 vya baraza la chini la bunge, na kuwa na wabunge wengi kuliko chama cha Republican. Uwingi huo unakipatia chama cha Democrat nguvu ya kudhibiti upitishaji wa sheria zinazohimizwa na serikali ya Rais Trump, kama ile ya bima ya afya, na mageuzi ya sheria ya uhamiaji.

  Chama cha Republican kinaendelea kuwa na udhibiti wa baraza la senate kwa kuwa na maseneta 51. Rais Trump aliandika kwenye ukurasa wa Tweeter kuwa uchaguzi umeleta mafanikio makubwa. Na kiongozi wa wabunge wa chama cha Democrat amesema ushindi wa chama chake wa kudhibiti baraza la chini utakiwezesha chama hiki kuidhibiti serikali ya Rais Trump.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako