• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 23 wa mawaziri wakuu wa China na Russia wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2018-11-08 09:44:58

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na mwenzake wa Russia Dmitry Medvedev wameendesha kwa pamoja mkutano wa 23 wa mawaziri wakuu wa China na Russia.

    Bw. Li Keqiang amesema China inapenda kushirikiana na Russia kuendelea kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa na kimkakati, kupanua ushirikiano wa pande zote, na kutoa mchango kwa ajili ya kulinda amani, utulivu na maendeleo ya dunia.

    Amesema mwaka huu ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Russia umeongezeka kwa haraka, thamani ya biashara inatazawa kuzidi dola za kimarekani bilioni 100, fursa za ushirikiano katika siku za mbele ni kubwa. Anatumai pande mbili zitaendelea kurahisisha biashara, kupanua uwekezaji, kuzidisha ushirikiano wa kilimo, na kuhimiza biashara ya kielekitroniki kati ya China na Russia.

    Bw. Medvedev amesema Russia inapenda kushirikiana na China kupanua biashara, kuongeza uwekezaji, kuharakisha kuanzisha mfuko wa uwekezaji katika sekta ya uvumbuzi, kuimarisha ushirikiano katika sekta za uvumbuzi, biashara ya kielekitroniki, kilimo, nishati, nishati ya nyuklia nausafirishaji na uchukuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako