• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washiriki wa maonyesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje wasifu fursa zinazotokana na maonesho hayo

    (GMT+08:00) 2018-11-08 16:51:26

    Washiriki wa Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya China wameisifu China kwa sera yake ya kufungua mlango zaidi na hatua za kuhimiza biashara huria duniani.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Idara la maendeleo ya biashara ya nje ya Malaysia Bw. Mohamed Shahreen Modros amesema, maonesho hayo yametoa nafasi kwa ukuaji wa biashara kati ya China na Malaysia, na kupongeza sera ya kufungua mlango zaidi.

    Naibu waziri wa biashara na viwanda wa Qatar Bw. Sultan bin Rashid al Khater amesema, maonesho hayo ni ishara ya China kwa dunia kuwa China sio tu inapata maendeleo yake, bali pia husaidia washirika kutimiza ufanisi wa uchumi.

    Meneja mkuu wa ofisi ya biashara ya nje ya Russia Bw. Andrey Slepnev amesema, maonesho hayo makubwa yamejenga jukwaa pana kwa ushirikiano wa biashara kati ya China na Russia, na kwamba kampuni kadhaa za Russia zimesaini mikataba ya ushirikiano na washirika wa biashara wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako