• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tunatakiwa kupata dunia ya kidigitali ya namna gani?

  (GMT+08:00) 2018-11-09 16:38:33

  Mkutano wa 5 wa kimataifa wa mtandao wa internet umefunguliwa kama ilivyopangwa huko Wuzhen, China. Kwenye mkutano huo wa siku tatu, washiriki walizungumza, kuwasiliana, kuonesha video na kujadili mada kuu ya mkutano ya "Kujenga dunia ya kidigitali iliyo ya uendeshaji wa pamoja na kuwa na hali ya kuaminiana ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwenye nafasi za mtandao wa internet, ambapo wameahidi kuchukua hatua kwa pamoja.

  Wiki moja kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, Kibanda kimoja cha kuuza magazeti huko Manhattan, New York, kilifuatiliwa sana na watu. Kwa kuwa jarida moja lililouzwa kwenye kibanda hicho linafanana sana na jarida lile maarufu, kisha watu wakaangalia kwa makini na kuona hata jina la jarida hili limebadilika pia, na vichwa vya habari kwenye ukurasa wa kwanza na jalada la jarida ni vya ajabu na vya kushangaza watu…kumbe hali ilikuwa ni kwamba, ofisi ya uhariri ya jarida la "Columbia Journalism Review" ilichapisha habari za uwongo zilizovuma sana kwenye mtandao wa huduma wa jamii kwenye jarida hili bandia lililojifanya kama ni la kweli, madhumuni yake ni kuwakumbusha watu wawe na macho juu ya uvumi wa habari za uwongo kwenye mtandao wa internet, na watu wakisoma jarida hili lililojifanya lile la kweli, wataona "kamusi" ya kuwafundisha wasomaji kutambua habari za uwongo.

  Ilipofika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, wasomaji wa mtandao wa internet wamezidi asilimia 55 duniani, watu karibu bilioni 4.2 wa duniani wanasoma habari kupitia mtandao, tena wamebadilisha njia yao ya kupata ujuzi, kubadilisha njia yao maisha na kufikiria, na kubadilisha mitazamo kuhusu maadili.

  Ndiyo maana, habari zinazotangazwa kwenye mtandao wa internet ni muhimu sana. Mtandao wa internet hauwezi kupiga marufuku ya kutangaza habari za maafa, ajali na kashfa, ama kufichua siri za mambo au za watu binafsi, au kama yanayoandikwa ni ya kweli au yalipakikana kwa njia halali, habari hizo zinaweza kutolewa kwenye mtandao ili kuvutia watu tu. Lakini sasa binadamu wanakabiliwa na hali halisi ambayo habari zinazoenea haraka zaidi kwenye mtandao ni za uongo, ambazo huwafanya watu waone shinikizo, huzuni na kutishwa. Mwanasayansi mwingereza wa kompyuta Tim Beners Lee aliyewahi kuvumbua mtandao wa Mesh, wakati wa kutimia miaka 30 ya mtandao wa internet, alisema amekata tamaa kuhusu hali ilivyo sasa ya maendeleo ya mtandao wa internet, ambao kampuni chache kubwa zinadhibiti haki zaidi, data za watu binafsi zinatumiwa ovyo, na hisia za chuki zinasambaa kwenye mtandao, hali hii inaruidisha nyuma sana na wazo lake la awali la kuvumbua mtandao. Na amesisitiza kuwa, mtandao wa internet unapunguza habari zinazoweza kuleta matumaini kwa watu, tena hauleti nguvu kwa watu binafsi, anaona mtandao wa internet unatakiwa kueneza ufuatiliaji na upendo zaidi kwa watu.

  Utafiti wa Chuo Kikuu cha teknolojia wa Massachusetts umeonesha kuwa, maoni hayo ya mwanasayansi Beners Lee kweli yanatokana na hali halisi, sasa uwezekano wa kunukuliwa kwa habari moja ya uwongo kwenye tweet unafikia zaidi ya asilimia 70; na kueneza habari za uwongo ni haraka zaidi kwa mara 10 hadi 20 kuliko kueneza habari zinazotokana na hali halisi. Na profesa mshiriki wa Chuo kikuu cha Colombia Taylor Owen, amesema mbali na kufuatilia habari zinazoenea kwenye mtandao, pia ni lazima kufuatilia muundo na njia ya kujipatia faida kwa shughuli za mtandao wa internet, hasa kampuni kubwa husika namna ya kukusanya data za watu binafsi kwa ajili ya kujipatia fedha. Amedhihirisha kuwa, haiwezekani kwa watu kutarajia kampuni hizo kubwa kutimiza lengo la kujisimamia. Ndiyo maana jumuiya ya kimataifa inalazimika kushirikiana katika kurekebisha na kukamilisha mfumo wa internet, ili mtandao huo uwe wazi na haki, na kuendelea kwa utaratibu.

  Hivi sasa binadamu wanaishi kwenye zama hizi za mtandao wa internet wenye uhai na mabadiliko zaidi, kwa vyovyote vile pande mbalimbali zinatakiwa kushiriki kwenye shughuli za kusimamia na kuendesha mtandao huo. Kama alivyosema Rais Xi Jinping wa China, nchi mbalimbali zinapaswa kujenga pamoja jumuiya ya mustakabali wa pamoja kwenye mtandao wa internet.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako