• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya makampuni ya China yanayoshughulikia ushirikiano wa uwezo wa uzalishaji viwandani nchini Kenya yafanyika Nairobi

    (GMT+08:00) 2018-11-09 20:09:19

    Baraza la China la Kukuza Biashara za Kimataifa CCPIT litafanya Maonesho ya makampuni ya China yanayoshughulikia ushirikiano wa uwezo wa uzalishaji viwandani nchini Kenya katika Kituo cha Mkutano wa Kimataifa wa Kenyatta kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 17 mwezi huu.

    Makampuni yatakayoshiriki kwenye maonesho hayo yataonyesha bidhaa za uzalishaji zenye ubora, ili kukidhi mahitaji ya kilimo cha kisasa na viwanda barani Afrika, kupanua soko la Afrika, na kuoanisha mipango minne ya maendeleo ya Kenya.

    Balozi mdogo anayeshughulikia mambo ya biashara wa China nchini Kenya Bw. Guo Ce amesema, China iko tayari kubadilishana uzoefu na mafanikio ya maendeleo, kuimarisha ushirikiano katika nyanja za uchumi, biashara na fedha na nchi za Afrika ikiwemo Kenya.

    Akizungumzia maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya China, Bw. Guo amesema kuwa kampuni za Kenya zilizoshiriki katika maonesho hayo zimesaini mikataba ya ushirikiano wa kibiashara yenye thamani ya mamilioni ya dola za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako