• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duru ya pili ya mazungumzo ya mambo ya diplomasia na usalama kati ya China na Marekani yafanyika

    (GMT+08:00) 2018-11-10 18:32:08

    Mjumbe wa Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China ambaye pia ni mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya diplomasia ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Yang Jiechi akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo na waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. James Norman Mattis huko Washington waliendesha kwa pamoja duru ya pili ya mazungumzo ya mambo ya diplomasia na usalama kati ya China na Marekani.

    Pande hizo mbili zilijadiliana kuhusu kazi za maandalizi ya kukutana kwa rais Xi Jinping wa China na rais Donald Trump utakaofanyika katika mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 nchini Argentina, na kufanya mawasiliano ya kutosha kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani na masuala makubwa ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa na pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako