• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya CIIE yaleta manufaa katika pande tatu, dunia kunufaika kwa muda mrefu

    (GMT+08:00) 2018-11-11 17:53:28

    Maonesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Uingizaji Bidhaa kutoka nje ya China CIIE yamefungwa jana mjini Shanghai. Jumla ya nchi 172, kanda na mashirika ya kimataifa, na zaidi ya makampuni 3600 yameshiriki kwenye maonyesho hayo ya siku sita, yaliyovutia zaidi ya wanunuzi wa ndani na nje wapatao 4000. Makubaliano ya kununua bidhaa na huduma yenye thamani ya dola bilioni 57.83 za kimarekani yamefikiwa kwenye maonyesho hayo.

    Matokeo hayo ni ya ajabu kwenye historia ya biashara duniani, watu wa nchi mbalimbali walioshiriki kwenye maonyesho hayo wamesema hawataki kuagana, na watakuja tena mwaka kesho.

    Maonyesho ya CIIE yalitangazwa na rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa kilele wa mwaka 2017 wa baraza la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ni uamuzi muhimu wa China kwa ajili ya kuhimiza duru mpya ya kufungua mlango, pia ni hatua muhimu ya China ya kufungua soko lake kwa dunia. Maonyesho hayo yameleta manufaa ya pande tatu, na yatanufaisha dunia kwa muda mrefu.

    Kwanza, maonyesho ya CIIE yamehimiza kufungua mlango, na kusaidia kurahisisha biashara na ongezeko la uchumi duniani.

    Pili, maonyesho hayo yamekusanya maoni ya pamoja, na kuhimiza dunia nzima kusonga mbele kwa mwelekeo mmoja wakati inapokabiliana masuala makuu ya uchumi na biashara. Tatu, maonyesho hayo yameonyesha wazo la "kujadiliana, kujenga kwa pamoja na kunufaishana", na kuyafanya yawe utekelezaji mzuri wa mtizamo wa "kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja".

    Kutokana na mpango wa China, maonyesho ya CIIE yatafanyika kila mwaka. Mpaka sasa makampuni zaidi 200 yamesaini makubaliano ya kushiriki kwenye maonyesho ya mwaka kesho. Hii inaonyesha kuwa, maonyesho ya CIIE yamekubaliwa na kukaribishwa na dunia. Katika siku za usoni, China itafanya juhudi katika kuongeza uwezo wake wa kununua bidhaa kutoka nje, legeza udhibiti wa kuingia katika soko, kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara, kujenga kiwango kipya cha kufungua mlango, na kuhimiza maendeleo ya kina ya ushirikiano wa pande mbilimbili na wa pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako