• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Mjasiriamali apata mkataba wa $2m kuuza pilipili China

    (GMT+08:00) 2018-11-12 19:43:35
    Mjasiriamali mdogo wa Rwanda,Diego Twahirwa, amesaini mktaba wa $2m wa kusafirisha mapipa 1,500 yaliyo na lita 37,500 za mafuta ya pilipili (Rwf1.7 bilioni).

    Utekelezwaji unaanza mwezi huu hadi Mei 2019.

    Mkataba huo ulifikiwa kati ya kampuni ya China ya Kai Jiang zi Wei Food na shamba la Gashora wakati wa maonesho ya uagizaji bidhaa ya China yaliyoandaliwa wiki iliyopita jijini Shanghai.

    Mkurugenzi Mkuu wa shamba la Gashora,Diego Twahira amesema kuwa wateja nchini China walifurahishwa na bidhaa yake ya pilipili wakisema kuwa ni mpya na bunifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako