• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China atoa makala kwenye vyombo vya habari vya Singapore

  (GMT+08:00) 2018-11-12 21:06:05

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa makala ya "kujenga mustakabali mzuri zaidi kwa kufungua mlango, ushirikiano na uvumbuzi" kwenye vyombo vya habari vya Singapore.

  Kwenye makala hiyo, Bw. Li amesema hii ni ziara yake ya kwanza nchini Singapore tangu ashike wadhifa wa waziri mkuu wa China. Mawasiliano na ushirikiano wa sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili vimeendelea kuzidishwa, na anatarajia nchi hizo mbili zitachukua maendeleo ya kila upande kama fursa ya kujiendeleza. Amesema kwa kupitia ushirikiano wa kunufaishana, nchi hizo mbili, hata nchi mbalimbali duniani zitatimiza maendeleo ya pamoja.

  Bw. Li amesisitiza kuwa, ili kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na kujilinda kibiashara na mfumo wa upande mmoja, nchi zote zinapaswa kushirikiana kulinda mfumo wa kibiashara wa pande nyingi wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), kuhimiza uhuru na urahisishaji wa biashara na uwekezaji, kutetea kwa pamoja, kutekeleza kihalisi na kushikilia kufungua mlango, na kujenga uchumi wa dunia wa ulio wazi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako