• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Singapore wakutana

    (GMT+08:00) 2018-11-13 14:44:23

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alizungumza na mwenzake wa Singapore Bw Lee Hsien Loong katika ikulu ya Singapore.

    Bw Li Keqiang amesema Singapore ni jirani mwema na mwenzi wa ushirikiano wa China. Nchi hizo mbili zina mustakbali na uwezo mkubwa wa ushirikiano, na makubaliano mengi yamefikiwa kwenye ziara yake. Amesema China inapenda kuendelea kuzidisha ushirikiano na Singapore, na kuimarisha kutoa mafunzo kwenye sekta za fedha, sayansi na teknolojia, na shughuli za makampuni.

    Bw Lee Hsien Loong amesema mafanikio mapya yamepatikana kwenye ushirikiano wa kiutendaji kati ya nchi hizo mbili. Marekebisho ya Makubaliano ya biashara huria ya Singapore na China yatayanufaisha makampuni na wananchi wa nchi zote mbili. Amesema Singapore inapenda kushirikiana na China katika kuhimiza ujenzi wa "Mji unaotumia teknolojia za kisasa" na ushirikiano wa biashara ya kidigitali, na kujenga njia mpya ya mawasiliano ya barabara na baharini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako