Maonyesho makubwa yameanza hapa Beijing katika kuadhimisha miaka 40 tangu China itekeleze sera ya mageuzi na kufungua mlango.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Wang Huning amezindua maonyesho hayo leo katika Jumba la Makumbusho la Taifa. Akizungumzia mabadiliko yaliyotokea katika miongo minne iliyopita, hususan mabadiliko ya kihistoria baada ya Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Wang amesema maonyesho hayo yanalenga kuonyesha mafanikio makubwa yaliyofanywa na watu wa China chini ya uongozi wa CPC katika njia ya ujamaa wenye umaalum wa Kichina.
Maonyesho hayo yanatumia picha za kihistoria, maandishi, video, na shughuli jumuishi ili kuwaonyesha wageni mchakato mkubwa ambao taifa la China limepitia, kuwa tajiri na kuwa lenye nguvu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |