Maonyesho makubwa yamezinduliwa leo katika Jumba la makumbusho ya taifa hapa Beijing, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 40 tangu China itekeleze sera ya mageuzi na kufungua mlango.
Rais Xi Jinping wa China leo mchana ametembelea maonyesho hayo, na kusisitiza kuwa maonesho hayo yanapaswa kutumika kuelimisha na kuongoza wananchi wa China kufahamu zaidi nguvu za chama cha kikomunisiti cha China (CPC), watu wa China na ujamaa wenye umaalum wa China, na kuelewa zaidi usahihi wa nadharia ya CPC, mpango wa kufanya mageuzi na ufunguaji mlango uliowekwa na kamati kuu ya CPC na mikakati mfululizo kuhusu mageuzi na ufunguaji mlango. Rais Xi amewataka Wachina kushikilia imani na nia ya kufuata kithabiti uongozi wa CPC katika njia ya ujamaa wenye umaalum wa China na njia ya mageuzi na ufunguaji mlango.
Maonyesho hayo yanatumia picha za kihistoria, maandishi, video, na shughuli jumuishi ili kuwaonyesha wageni mchakato mkubwa ambao taifa la China limepitia, kuwa tajiri na kuwa lenye nguvu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |