• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China atoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Singapore

    (GMT+08:00) 2018-11-14 09:48:02

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa mwito wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Singapore.

    Bw. Li ambaye yuko ziarani nchini Singapore, alisema hayo jana alipoongea kwenye tafrija ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Shirikisho la biashara Singapore na Baraza la biashara na viwanda kati ya Singapore na China.

    Bw. Li Keqiang amesema China iko tayari kushirikiana na Singapore kuanzisha majukwaa ya ushirikiano kwa ajili ya muunganiko, uungaji mkono wa kifedha na ushirikiano wa upande wa tatu, ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kibiashara na kifedha kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Li pia amesisitiza kuwa China itaendelea kupunguza urasimu kwenye utawala, kupunguza kodi na kuweka mazingira ya kibiashara yenye ushindani wa haki, yatakayowatendea kwa usawa wafanyabiashara wa China na nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako