• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbao na Bandari FC zaingizwa kwenye michuano

    (GMT+08:00) 2018-11-14 10:19:17
    timu ya Mbao fc ya Tanzania na Bandari fc ya Kenya zimeingizwa rasmi kwenye orodha ya timu nane zitakazoshiriki michuano ya kuwania kombe la SportPesa itakayofanyika mwakani nchini Tanzania.

    michuano hiyo ilizinduliwa mwaka 2017 nchini Tanzania huku mshindi wa michuano hiyo timu ya Gor Mahia ya Kenya alikutana na timu ya Everton ya Uingereza jijini Dar es salaam kabla ya timu hizo kukutana tena mwaka huu jijini London Uingereza.

    Michuano ya SportPesa ya mwakani itashirikisha timu za Simba, Yanga, Singida United na Mbao kutoka Tanzania, huku Kenya itawakilishwa na timu za Gor Mahia, AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Bandari fc.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako