• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ahudhuria mkutano wa pili wa viongozi wa RCEP

    (GMT+08:00) 2018-11-15 14:11:26

    Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang jana amehudhuria mkutano wa pili wa viongozi wa makubaliano ya ushirikiano wa wenzi wa kiuchumi wa pande zote wa kikanda RCEP nchini Singapore. Viongozi wa Umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki ASEAN na wengine kutoka Korea Kusini, Japan, Australia, New Zealand na India wameshiriki kwenye mkutano huo.

    Bw Li amesema hivi sasa mazungumzo yapo katika kipindi muhimu, juhudi zaidi zinatakiwa kufikia makubaliano hayo ndani ya mwaka ujao, ili kuongeza uhuru na urahisi wa biashara na uwekezaji, kuhimiza mafungamano ya kiuchumi ya kikanda, na kuwanufaisha watu wa kanda hiyo mapema iwezekanavyo.

    Viongozi wanaohudhuria mkutano huo wameona pande zote husika zinapaswa kujitahidi katika kuhimiza mafungamano ya kiuchumi, na kusukuma mbele biashara huria na utaratibu wa kimataifa unaofuata kanuni. Kufikiwa kwa makubaliano hayo ya RCEP kunaweza kusaidia kujenga imani na matarajio mazuri, na kuhimiza ukuaji wa uchumi wa kikanda na mafungamano ya kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako