• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Real Madrid yawanyapia Neymar na Mbappe, PSG yachunguzwa na UEFA

  (GMT+08:00) 2018-11-16 09:25:20

  Klabu ya Real Madrid ipo tayari kuipatia Paris Saint-Germain (PSG) kitita kinono cha fedha endapo itakubali kuwauza wachezaji wake Neymar au Kylian Mbappe ili kuepuka sheria za Chama cha soka barani Ulaya dhidi ya udhibiti wa fedha (FFP).

  UEFA ilianzisha sheria ya fedha ili kudhibiti klabu kutofanya matumizi makubwa zaidi kuliko kile wanachokiingiza hali ambayo itapelekea kutumbukia kwenye janga la kiuchumi.

  Kitendo cha klabu ya PSG kufanya usajili mkubwa kwa wachezaji wake wawili, Neymar iliyowagharimu pauni milioni 200 na Mbappe pauni milioni 166 kinawaweka chini ya uchunguzi wa UEFA kupitia sheria hiyo ya fedha. Madrida wamekuwa wakisaka saini ya nyota hawa kwa udi na uvumba baada ya kumuuza staa wao Cristiano Ronaldo kwenda Juventus

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako