• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema baraza kuu la Umoja wa Mataifa lapaswa kujadili masuala muhimu yanayofuatiliwa na nchi wanachama wengi

    (GMT+08:00) 2018-11-16 19:47:58

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, baraza kuu la Umoja huo linapaswa kujadili na kukabiliana na masuala yanayofuatiliwa na nchi wanachama wengi, hasa yale yanayohusiana na maslahi ya nchi zinazoendelea.

    Bw. Wu amesema hayo katika mjadala wa pamoja wa baraza kuu la 73 la Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa azimio la Umoja huo na ajenda ya "Kustawisha baraza kuu". Amesema, baraza kuu la Umoja wa Kimataifa ni idara kuu inayoanzishwa kwa mujibu wa katiba ya Umoja wa Mataifa, ambayo ina jukumu la kupitisha sera. Kustawisha baraza kuu linahusiana na maslahi ya nchi wanachama wote, pia kutaleta athari muhimu na ya muda mrefu kwa kuongeza mamlaka na uaminifu wa Umoja huo.

    Bw. Wu pia amesema, baraza hilo linapaswa kushirikiana na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuimarisha uratibu na ushirikiano katika masuala yanayohusiana na amani na usalama wa kimataifa kwa mujibu wa katiba ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako