• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda kupambana na ongezeko la ajali za barabarani

    (GMT+08:00) 2018-11-19 09:01:14

    Mamlaka nchini Rwanda zimesema zitawachukulia hatua kali wanaokiuka kanuni za usalama barabarani, ili kupambana na ajali za barabarani zinazoongezeka kote nchini humo.

    Waziri wa nchi anayeshughulikia uchukuzi katika wizara ya miundombinu Bw. Jean de Dieu Uwihanganye, amesema sheria mpya ya usalama barabarani itakayotolewa hivi karibuni, itatoa adhabu kali kwa watu wanaokiuka kanuni za usafiri barabarani, na ametoa wito kwa polisi wa usalama barabarani na mashirika yote ya uchukuzi kushirikiana katika kurejesha utaratibu na usalama wa barabarani nchini Rwanda.

    Takwimu zinaonesha kuwa, kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, ajali za barabarani zilizotokea nchini humo zimesababisha vifo vya watu 437, na wengine 662 wamejeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako