• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Brunei kuimarisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati

    (GMT+08:00) 2018-11-19 18:19:37

    Mwanzoni mwa mwaka 2018, benki za Citi na HSBC zilisitisha shughuli zao za kifedha nchini Brunei. Habari zilizotolewa na gezeti la Asia Times zilisema, kutokana na kupungua kwa bei ya nishati duniani katika miaka ya karibuni, biashara za mafuta na gesi za benki hizo nchini Brunei pia ziliathirika.

    Brunei ni nchi kubwa ya tatu katika Asia Kusini Mashariki inayozalisha mafuta na ni nchi kubwa ya nne duniani inayozalisha gesi ya asili, na sekta ya mafuta na gesi inachukua asilimia 60 ya uchumi wake. Katika miaka ya karibuni, uchumi wa Brunei umeathirika vibaya. Brunei imetoa mkakati wa maendeleo wa "Malengo 2035", ili kutafuta maendeleo ya uchumi unaoshirikisha pande nyingi.

    Wakati wawekezaji wa nchi nyingine walipoanza kuondoka nchini Brunei, China iliiunga mkono nchi hiyo. Mwaka 2016 Benki ya China ilianzisha ofisi yake nchini Brunei, na kutoa msaada kwa wawekezaji kutoka China.

    China na Brunei zilianzisha uhusiano wa kibalozi mwaka 1991, lakini mwaka 2013 nchi hizo mbili ziliamua kuinua uhusiano wao na kuwa wa ushirikiano wa kimkakati. Mwaka huo rais Xi Jinping wa China alitoa pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na Brunei ilieleza kuunga mkono pendekezo hilo. China na Brunei zilisaini makubaliano ili kuhimiza mafungamano ya pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na Malengo 2035. Pendekezo hilo limetilia nguvu mpya ya uhai kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Brunei pamoja na nchi nyingine za Umoja wa Asia Kusini Mashariki zimekuwa nchi wanachama walioanzisha Benki ya uwekezaji wa miundo mbinu ya Asia.

    Katika miaka ya karibuni, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Brunei umepata maendeleo ya kasi. Mwaka 2017 thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili iliongezeka kwa asilimia 36.5, na kufikia dola za kimarekani bilioni moja. Thamani ya usafirishaji bidhaa ya Brunei nchini China iliongezeka kwa asilimia 58.8.

    Hivi sasa kampuni nyingi zaidi za China zimeanza kuwekeza nchini Brunei. China pia inafanya juhudi kushiriki kwenye ujenzi wa miundo mbinu nchini Brunei. Nchi hizo mbili pia zinaimarisha mawasiliano ya jamii na utamaduni. Mwaka jana idadi ya watalii kutoka China nchini Brunei ilifikia elfu 52, na kuweka kiwango cha juu cha kihistoria.

    Rais Xi Jinping wa China yupo ziarani nchini Brunei tarehe 19 na 20. Kwenye taarifa ya pamoja ya nchi hizo mbili, rais Xi na Sultani Haji Hassanal Bolkiah waliamua kuinua uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kutoka uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati. Uamuzi huo hakika utahimiza zaidi uhuisiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako