• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Kenya yazima shambulizi la kundi la Al Shabaab kwenye mji wa mpakani wa Garissa

    (GMT+08:00) 2018-11-19 19:04:49

    Polis nchini Kenya wamefanikiwa kuzima shambulizi lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab katika kambi ya polisi iliyoko Ijara kwenye kaunti ya Garissa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Kamishna wa polisi wa kanda ya Kaskazini Mashariki Mohamed Birik amefafanua kuwa, mpiganaji mmoja wa kundi la Al Shabaab ameuawa na wengine kadhaa wametoroka wakiwa na majeraha makubwa waliyopata wakati wa shambulizi hilo.

    Polisi wamesema, wapiganaji hao walitaka kufanya mashambulizi mawili kwa wakati mmoja, kushambulia kituo cha polisi na wakati huo huo kuharibu mnara wa mawasiliano wa kampuni ya simu ya Safaricom.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako