• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Botswana yakaribisha uwekezaji zaidi wa kampuni za China

    (GMT+08:00) 2018-11-19 19:05:11

    Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Botswana Bogolo Kenewondo amesema, nchi hiyo inakaribisha uwekezaji zaidi wa China ili kusaidia kutimiza Ruwaza ya mwaka 2036 ya nchi hiyo.

    Akizungumza kwenye kumbukumbu ya miaka 30 ya uwepo wa kampuni ya ujenzi ya China (CSCEC) nchini humo, Bw. Kenewondo amesema nchi hiyo inadhamiria kutafiti fursa zilizotolewa na Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kwa kuwa nchi hiyo inadhamiria kujitoa kwenye hadhi ya uchumi wa kati na kuwa na uchumi wa juu.

    Amesema watatumia ahadi za FOCAC kuhusu urahisishaji wa biashara kuongeza biashara kati ya nchi hiyo na China, ili kuimarisha zaidi uhusiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako