• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe awataka viongozi wa Afrika kupambana na rushwa

    (GMT+08:00) 2018-11-19 19:05:33

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema ni muhimu kwa nchi zote za Afrika kupambana na ufisadi ndani ya sheria zao, kwa kuwa kuanzishwa kwa Eneo la Biashara Huria la Afrika limeanzisha uchumi mmoja barani humo wenye soko lenye watu bilioni 1.2.

    Rais Mnangagwa amesema hayo alipowasili Harare akitokea kwenye Kikao Maalum cha Mkutano wa Umoja wa Afrika kilichofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambacho kilijadili mapendekezo ya mageuzi ya kubadili taasisi hiyo iwe yenye ufanisi zaidi na yenye uwezo wa kuleta utulivu na ustawi wa kiuchumi katika bara hilo.

    Amesema kuna haja kubwa ya kubadili mfumo wa Umoja wa Afrika ili uafikiane na mageuzi ya kisasa, kutoka kufuatilia masuala ya kisiasa na kujikita kwenye maendeleo ya uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako