• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio ya uhalifu visiwani Zanzibar yapungua kwa asilimia 34

    (GMT+08:00) 2018-11-20 08:56:16

    Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema matukio ya uhalifu yamepungua kwa asilimia 34 katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu.

    Rais Shein amesema hayo wakati waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Bw. Kangi Lugulo na maofisa wengine waandamizi walipotembelea Ikulu ya Zanzibar. Amepongeza juhudi zilizofanywa na wizara ya mambo ya ndani na kusema mwendelezo wa juhudi zinazofanywa na idara ya usalama nchini humo zimeleta amani na masikilizano visiwani Zanzibar.

    Waziri wa mambo ya ndani Bw. Lugola amemhakikishia rais Shein kuwa wizara yake itaendeleza juhudi ili kudumisha amani na usalama visiwani Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako