• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wahimiza kutolewa kwa vitambulisho vya kidijitali wakati watu milioni 500 wa Afrika hawana vitambulisho rasmi

    (GMT+08:00) 2018-11-20 08:56:34

    Kamisheni ya kiuchumi kwa Afrika ya Umoja wa Mataifa ECA imesema watu wapatao milioni 500 barani Afrika hawana vitambulisho rasmi (ID), hali inayochangia kuachwa nyuma kwa mamilioni ya waafrika.

    Taarifa hiyo ilitolewa na katibu mtendaji wa ECA Bibi Vera Songwe, ambaye pia amewataka viongozi wa Afrika kuchukua hatua mwafaka kuhimiza kutolewa kwa vitambulisho vya kidijitali kwenye mkutano wa ngazi ya juu uliofanyika Jumapili kando ya Mkutano wa kilele wa 11 wa Umoja wa Afrika uliofungwa wikiendi iliyopita mjini Addis Ababa.

    Bibi Songwe amesema Jukwaa la utambulisho wa kidijitali kwa Afrika litahakikisha kuwa mashirika madogo na yenye ukubwa wa kati ambayo yanachukua asilimia 80 ya mashirika yote ya Afrika, yananufaika na fursa hii, na kwamba vitambulisho vya kidijitali ni chombo muhimu wezeshi kwa raia kupata huduma za kijamii na kisiasa, na kushirikishwa kwenye shughuli za kifedha na kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako