• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi Tanzania wachukua hatua kupambana na ajali za barabarani

    (GMT+08:00) 2018-11-20 08:56:56

    Polisi nchini Tanzania wameanzisha programu mpya ya kuwarudisha shuleni madereva wasiotimiza vigezo vya kiuwezo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza ajali za barabarani nchini humo.

    Kamanda wa polisi kanda ya Arusha Bw. Joseph Bukombe amesema programu hiyo imekuja ikiwa ni moja ya hatua za kupunguza ajali za barabarani, ambazo asilimia kubwa zimesababishwa na kuendesha magari kwa uzembe.

    Bw. Bukombe amesema madereva wengi walipata leseni za kuendesha magari kwa njia haramu bila kupita kwenye utaratibu rasmi, na hivyo kuendesha magari bila kuwa na uwezo unaohitajika.

    Kamanda huyo amesema chini ya programu hiyo, madereva wote wasiopewa mafunzo kama wanavyotakiwa watapelekwa kwenye mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi VETA, ambako watapewa mafunzo ya kuendesha magari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako