• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakulima wa korosho wafurahia jasho lao huku vyama vya ushirika vikiwa taabani.

    (GMT+08:00) 2018-11-20 19:05:25

    Wakati Serikali ikianza kuwalipa wakulima wa korosho fedha bila makato yoyote, vyama vikubwa vya ushirika mkoani Mtwara vimesema vitashindwa kujiendesha kwa kukosa mgao vinaostahili kutoka katika malipo ya korosho. Kufikia sasa, serikali imewalipa zaidi ya wakulima 2000 kutoka vyama 35 vya ushirika vilivyohakikiwa, huku ikiendelea na uhakiki na kufanya malipo.

    Serikali ilifikia uamuzi wa kununua korosho kwa Sh3,300 baada ya wakulima kugomea minada ya awali iliyokuwa na bei chini ya Sh3,000 kwa kilo. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliingilia kati suala hilo, lakini wafanyabiashara wachache waliojitokeza walinunua korosho kidogo na bei juu kidogo ya Sh3,000.

    Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa vyama vya ushirika vya Tandahimba na Newala (Tanecu) na chama cha Masasi na Nanyumbu (Mamcu), walisema wamekuwa wakijiendesha kupitia makato hayo ya mauzo ya korosho, ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara ya wafanyakazi na kutekeleza miradi ya maendeleo.

    Mwenyekiti wa Tanecu, Mohamed Nassoro ameambia gazeti la Mwananchi kuwa chama hicho kilitarajia kukusanya Sh3 bilioni baada ya kukata Sh30 kwa kila kilo moja katika zaidi ya tani 100,000 walizokusanya. Alisema tayari wameshazungumza na Waziri wa Kilimo, Japheth Hasunga na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika, lakini hawajafikia mwafaka.

    Maelezo kama hayo yalitolewa pia na mwenyekiti wa Mamcu, Protency Rwiza akisema mpaka sasa hawajui chama hicho kitajiendeshaje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako