• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda; Wafanyibiashara wa wadogo na wastani wasema hawajawahi kupewa motisha

    (GMT+08:00) 2018-11-20 19:06:14

    Ukosefu wa habari muhimu ya biashara inawadhuru sana wafanyibiashara wadogo na wale wa wastan kutoka eneo la Fort Portal. Wafanyibiashara hawa waliokuwa na kongamano mjini Fort Portal, walijadiliana masaibu na changamaoto wanazokumbana nazo wakiwa kazini na kuomba wahusika wakuu wa kutetea maslahi yao kuwanusuru. Mojawapo ya tatizo kuu ni kukosa vyeti vya kuthibitisha uhalali wa kazi zao. Wanaomba Shirika la Viwango vya Bidhaa la Uganda kutatua swala hili.

    Swala la ulipaji ushuru pia lilijadiliwa kwa kina. Wafanyibiashara hawa wanasema kwamba wamelazimika kulipa ushuru hata endapo biashara zenyewe hazileti faida yoyote. Aidha ilibainika kuwa baadhi ya wafanyibiashara hawa vile vile hawajui endapo kuna mipango maalum ya serikali ya kuwasaidia. Kwa mfano, utoaji mafunzo na mikopo kwa wafanyibiashara wa kiwango hiki cha chini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako