• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maelfu ya wageni watazama maonesho ya maadhimisho ya miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango

  (GMT+08:00) 2018-11-20 19:57:53

  Maelfu ya wageni kutoka nchi mbalimbali wakiwemo mabalozi, wataalamu na wajumbe wa idara za kibiashara jana wamealikwa kwenye maonesho ya "Maadhimisho ya miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango" yaliyofanyika kwenye jumba la makumbusho la taifa la China hapa Beijing. Wageni hao wamesema tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, imepata maendeleo ya kuishangaza dunia, na wanatarajia kushirikiana zaidi na China ili kunufaika na kupata mafanikio kwa pamoja.

  Kwenye jumba la maonesho, konsela mkuu wa ubalozi wa Pakistan nchini China Bw. Raheel Tariq amejaribu mfano wa kuendesha treni ya kasi ya "Fuxing", alimwambia mwandishi wetu wa habari kwamba amevutiwa na maendeleo ya China katika usafirishaji, uchumi wa kitarakimu na teknolojia ya mtandao wa Internet, akisema,

  "Nimefurahi kujionea jinsi China ilivyopata maendeleo ya kasi na uchumi wa China ulivyoongezeka, huu kweli ni muujiza. Pakistan inaweza kujifunza uzoefu mwingi wa China. Nina matumaini kwamba China na Pakistan zitafanya ushirikiano katika pande nyingi zaidi, ili kunufaishana na kupata mafanikio kwa pamoja."

  Kwenye maonesho hayo, sanamu ya wanakijiji 18 wa kijiji cha Xiaogang mkoani Anhui China walioamua kugawanya mashamba ya kijiji kwa kila familia ya wakulima na kufungua ukurasa wa mageuzi ya vijiji nchini China, na mifano ya roketi aina ya Long March na kituo cha anga ya juu cha Tiangong si kama tu yameonesha mafanikio ya sera ya mageuzi na ufunguaji mlango nchini China, bali pia yameonesha kuwa busara na mipango ya China inanufaisha nchi na watu wengi duniani, kupitia wazo la kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu wote. Katibu wa ngazi ya kwanza wa ubalozi wa Uruguay Bibi Chenoa amesema sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ina umuhimu wa kimkakati kwa China, na ana imani kubwa kuhusu maendeleo ya China katika siku zijazo, akisema,

  "Hayo ni maonesho mazuri, tunatakiwa kuelewa zaidi historia na mafanikio ya China. Maendeleo ya China yameishangaza dunia, nimevutiwa zaidi na maendeleo ya China katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia."

  Habari zinasema maonesho hayo yamegawanyika katika sehemu 6, ambazo zinaonesha mabadiliko ya uzalishaji na maisha ya umma wa China katika miaka 40 iliyopita, hasa baada ya mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako