• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TOC yaonya wanamichezo Olimpiki

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:04:28
    Licha ya kutengewa dola milioni 1 za maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki mwaka 2020 nchini Japan, kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imesema kama wanamichezo wa Tanzania hawatofikia viwango ambavyo vimeweka, itakuwa ni ndoto kupata mgao wa fedha.

    Hivi karibuni chama cha kamati ya Olimpiki Afrika (ANOCA) kilitangaza kutenga fedha hizo kwa ajili ya maandalizi ya timu za riadha, judo, kunyanyua vitu vizito, ngumi, tenisi na kuogelea.

    Katibu mkuu wa TOC. Filbert Bayi amesema ANOCA inataka mchezaji ambaye ataandaliwa kwa kutumia fedha hizo awe ni namba tatu kwa ubora Afrika na namba 10 duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako