• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha mkuu afunguka kufugwa kwa timu ya Zanzibar michezo ya klabu bingwa

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:07:16
    Kocha mkuu wa timu ya taifa za mpira wa mikono ya Zanzibar Kombo Ali Kombo amezugumzia sababu ya kushindwa kwa timu za Zanzibar kwenye michezo ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati yaliomalizika Zanzibar kwenye viwanja vya jeshini Nyuki.

    Amesema mashindano hayo yamemaliza lakini hayakuwa mazuri kwa Zanzibar licha ya mashindano kuwa ni ya ushindani ila vilabu vya Zanzibar havikufanya vizuri kwenye mashindano hayo kutokana na kukosa mashindano ya Kimataifa na uwezo wa kucheza mchezo huo kwenye kiwango cha kimataifa.

    Mashindano ya mpira klabu bingwa Afrika mashariki ya mpira wa mikono yamemalizika Zanzibar huku Polisi ya DRC wamefanikiwa kuwa mabingwa wa mashindano haya baada ya kuifunga Black Mamba kutoka Kenya magoli 23 kwa 17 na kupatiwa medali ya Dhahabu na Kombe .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako