• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yadhamiria kujiunga na OECD ili kuvutia uwekezaji duniani

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:26:52

    Rwanda imeeleza dhamira yake ya kujiunga na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo OECD ikiwa sehemu ya juhudi za kuvutia uwekezaji duniani.

    Akiongea na wanahabari jana mjini Kigali, waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Bw. Richard Sezibera amesema Rwanda inatarajia kuomba rasmi uanachama wa OECD na ina uhakika itakubaliwa. Rwanda imekuwa ikifanya mageuzi mengi yanayoiwezesha nchi kufanya vizuri kwenye ripoti ya biashara ya Benki ya Dunia.

    OECD likiwa ni shirika la maendeleo ya kiuchumi kati ya serikali lenye nchi wanachama 36, lilianzishwa mwaka 1961 likiwa na lengo la kuchochea maendeleo na biashara duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako