• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waitaka Afrika kutoa kipaumbele sekta ya viwanda kwa ajili ya maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:40:56

    Umoja wa Mataifa umezitaka serikali za Afrika kutoa kipaumbele kwa sekta ya viwanda ili kutimiza maendeleo endelevu.

    Kwenye sherehe ya kuadhimisha siku ya maendeleo ya viwanda barani Afrika, mwakilishi wa shirika la maendeleo ya viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO nchini Kenya, Eritrea, Sudan Kusini, Comoros na Shelisheli Bw. Emmanuel Kalenzi, jana huko Nairobi alisema katika siku zilizopita, bara la Afrika lilizingatia zaidi sekta za kijamii, kama vile elimu na afya, serikali za Afrika zinapaswa kutoa kipaumbele kwa sekta za uzalishaji kama vile sekta ya viwanda, kwa sababu zinatoa ajira, bidhaa na huduma, ambazo zitahitajika kwa sekta nyingine.

    Siku ya Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika AID iliyowekwa mwaka 1989na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, inalenga kuwashirikisha viongozi wa Afrika na kuhamasisha ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya viwanda ya bara hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako