• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM aomba uungaji mkono kwa kazi za kulinda amani barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-11-21 09:58:49

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameomba uungaji mkono katika kusaidia kudumisha amani barani Afrika. Amesema, mapambano barani Afrika yanatishia usalama wa dunia.

    Bw. Guterres amesema kwenye Baraza la Usalama la umoja huo kuwa, sababu za mapambano barani Afrika ni umaskini, ukosefu wa ajira kwa vijana, mabadiliko ya hali ya hewa, kugombea raslimali na uhalifu wa kimataifa. Pia amesema kuongeza ufanisi wa kazi za kulinda amani barani Afrika ni jukumu la jumuiya ya kimataifa.

    Amesema uwezo wa Umoja wa Mataifa katika suala hilo hautoshi, hivyo ni muhimu kwa operesheni zote za kulinda amani zinazoongozwa na Afrika chini ya mamlaka ya baraza hilo, zipatiwe misaada ya fedha endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako