• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto kwa kuahidi kuboresha elimu na usalama kwa watoto

    (GMT+08:00) 2018-11-21 18:06:54

    Kenya imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto hapo jana na kurejea tena ahadi yake ya kuboresha upatikanaji wa elimu na usalama kwa watoto.

    Waziri wa elimu nchini humo Bi. Amina Mohamed amesema, sera chanya zimewekwa ili kuboresha uandikishwaji wa watoto katika shule, na kwamba tayari wameweka wazi hatua zinazohitajika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu ya lazima ya msingi.

    Bi. Mohammed amesema Kenya imewekeza katika maeneo yaliyolengwa ili kuhakikisha kuwa kuwawezesha watoto kunatimizwa kupitia elimu na upatikanaji wa huduma muhimu kama vile afya, makazi, na lishe bora. Amesema serikali inafuatilia sana elimu ya awali ili kuhakikisha inaendana na mahitaji ya kimwili na kiakili ya watoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako