• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ziara ya rais Xi Jinping ya kuhudhuria mkutano usio rasmi wa APEC imesukuma mbele mwelekeo wa ufunguaji mlango na ushirikiano

  (GMT+08:00) 2018-11-21 18:08:26

  Kuanzia tarehe 15 hadi 21 Novemba, rais Xi Jinping wa China alihudhuria mkutano usio rasmi wa 26 wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya Asia na Pasifiki APEC, kufanya ziara ya kiserikali nchini Papua New Guinea, Brunei na Philippines, na kukutana na viongozi wa nchi nane za visiwa zenye uhusiano wa kidiplomasia na China.

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema katika ziara hiyo rais Xi Jinping alijadiliana na wajumbe wa APEC kuhusu mafungamano ya uchumi wa kanda hiyo, kujadiliana na viongozi wa nchi za Asia Kusini kuhusu ushirikiano wa kimkakati, na kutunga mpango wa maendeleo endelevu na viongozi wa nchi za visiwa. Ziara hiyo inalenga kupendekeza wazo la kujenga jumuiya ya binadamu wote yenye mustakabali wa pamoja, kuimarisha ushirikiano wa kiwenzi, kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuimarisha nia kuhusu kuanzisha mfumo wa pande nyingi, kufikia maoni ya pamoja na kuongeza nguvu ya kutimiza maendeleo ya pamoja. Wakati vitendo vya kujilinda kibiashara, vitendo vya upande mmoja na utawala kwa nguvu vinaporudishwa duniani, China siku zote inashikilia kupata mafanikio kwa pande mbili, pande zote na kwa pamoja, kushikilia kujadiliana, kujenga na kunufaika kwa pamoja, na imeonesha kuwa China ni nchi kubwa yenye moyo wa kiujenzi, inayowajibika na inayotilia mkazo maadili na haki.

  Bw. Wang Yi amesema wakati hali zisizo tulivu zinaongezeka kwenye uchumi wa dunia, kanda ya Asia na Pasifiki ikiwa ni injini muhimu ya ongezeko la dunia imefuatiliwa na watu wengi. Rais Xi Jinping alipohudhuria mkutano wa APEC, amechambua kwa kina changamoto ya jumuiya ya kimataifa, na kutoa mipango na busara ya China kwa maendeleo na ushirikiano wa uchumi wa kanda hiyo na duniani. Bw. Wang Yi pia amesema, ziara ya rais Xi Jinping imeimarisha urafiki wa jadi kati ya China na nchi jirani, na kuinua uhusiano kati China na Brunei na Philippines.

  Bw. Wang Yi ameongeza kuwa rais Xi Jinping kufanya ziara ya kwanza nchini Papua New Guinea na kukutana tena na viongozi wa nchi za visiwa baada ya miaka minne, ni muhimu kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na nchi za visiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako