• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza kuweka vikwazo kwa mashirika na watu binafsi tisa wa Iran na Russia

    (GMT+08:00) 2018-11-21 18:50:59

    Wizara ya fedha ya Marekani imetangaza kuweka vikwazo kwa mashirika na watu binafsi tisa wa Iran na Russia ambao wanashukiwa kuiuzia mafuta serikali ya Syria.

    Aidha wizara hiyo imeyaonya makampuni ya usafirishaji wa bidhaa kwa meli yasisafirishie mafuta serikali ya Syria, ama sivyo yatakabiliwa na hatari kali. Naibu waziri wa fedha ya Marekani Bw. Sigal Mandelker amesema, nchi hiyo itaendelea kuweka vikwazo kwa pande zinazosaidia kuiuzia mafuta Syria na kusaidia Iran kukwepa vikwazo vya Marekani.

    Kwa mujibu wa sheria husika za Marekani, mali za watu walioadhibiwa nchini humo zitashikiliwa, na wananchi wa Marekani hawaruhusiwi kufanya nao biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako